Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mazungumzo ya amani ya Syria yamechukua mkondo mpya juu ya hatima ya rais Bashar al Assad huku wanamgambo wa Hezbollah wakiapa kupambana sambamba na vikosi vya serikali ili kuwashinda nguvu magaidi wa Daesh ambao wanaungwa mkono na Saudia arabia na Marekani kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria.
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa kwaajili ya Syria Staffan de Mistura, amesema amejaribu kuipa shinikizo Syria kuweka wazi hatua yake juu ya suala la suluhu ya kisiasa, huku mazungumzo hayo ya amani yanayofanyika mjini Geneva Uswisi yakiingia wiki yake ya pili.
De Mistura amesema mjumbe anayeongoza majadiliano upande wa Syria Bashar al-Jaafari amemuambia ni mapema sana kuzungumzia jambo hilo, huku akiongeza kuwa mustakbal wa Assad na suala la suluhu la kisiasa ni mambo mawili tofauti. Bashar amesema rais Assad hahusiki kwa njia yoyote ile na mazungumzo yanayoendelea Geneva akisisitiza kuwa suala la rais huyo ni kitu kilichotolewa zamani katika ajenda ya mazungumzo na kwamba rais Assad ataendelea kuwa rais.
Aidha hatma ya rais Bashar al Assad imekuwa kizingiti katika mazungumzo ya hivi karibuni yanayonuiwa kumaliza mapigano nchini humo yaliyoingia mwaka wake wa tano, na yaliyosababisha mauaji ya zaidi ya raia 270,000 na kuwaacha mamilioni ya wengine bila makaazi. Upinzani unasisitiza ni lazima Assad aondoke madarakani ili muafaka juu ya mzozo huo uweze kupatikana.
Serikali za Marekani, Uturuki, Saudia arabia na washirika wao wamekuwa wakitumia makundi ya kigaidi kwa kuyapa silaha na misaada ili yaangushe utawala wa Syria lakini juhudi hizo za kishetani zimeishia ukingoni baada ya majeshi ya Iran na Urusi kuingilia kati na kuwatetea wananchi wa Syria ambao wanauawa bila hatia.
Hata hivyo hatua ya kusimamisha mapigano kwa muda iliyoanza kutekelezwa mwezi uliyopita imetoa matumaini ya kumalizika mapigano hasa wakati Urusi, mshirika mkuu wa rais Assad ilipotangaza kuondoa majeshi yake yote nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kuelekea Urusi kuijadili Syria
Lakini hali ya wasiwasi imerejea tena baada ya Marekani kuendelea kuwatetea magaidi wanao endeleza mashambulizi dhidi ya serikali na wananchi wa Syria katika kipindi hiki cha kusimamisha vita, jambo lilipelekea Urusi kutoa onyo kwa Marekani kuwa nchi hiyo itarudisha majeshi yake nchini Syria na kuendelea kuwaangamiza magaidi wanaodhaminiwa na Marekani, Suala hili ndio limepelekea Marekani kumtuma waziri wake wa mambo ya nje kwenda kujaribu kuituliza Urusi isianzishe mashambulizi dhidi ya magaidi hao.
Kumekuwa na wasiwasi mwengine pia wa iwapo makubaliano yoyote ya mani yanaweza kufikiwa katika uwanja wa mapambano nchini Syria kufuatia wanamgambo wa Hezbolla kusema watabakia nchini Syria hadi watakapowashinda magaidi wa Daesh wanaodhaminiwa na Saudia arabia na Marekani.
"Yale yote yaliyosemwa kuhusu sisi kuondoka Syria ni uwongo mtupu, tulikwenda Syria kuisaidia nchi hiyo kutoanguka mikononi mwa magaidi wa Daesh na makundi mengine ya kigaidi, kama tuna wajibu wa kuwa huko tutaendelea kuwa huko," alisema kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.
Mwisho wa habari/ 291